Chama
cha NCCR-Mageuzi kimeendelea kuigaragaza CCM mahakamani, baada ya Mbunge wa
Kasulu Vijijini, Mhe. Agripina Zaituni Buyogela (pichani), kuibuka kidedea kwenye rufaa ya kupinga
matokeo ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010, yaliyompa ushindi.
Hiyo
ni mara ya pili kwa Buyogela, kuibuka kidedea dhidi ya aliyekuwa Naibu Waziri
wa Habari, Utamaduni na Michezo, Daniel Nsanzugwanko, aliyekuwa akigombea kiti
hicho kupitia CCM.
Nsanzugwanko,
alifungua kesi Mahakama Kuu Kanda ya Tabora akipinga matokeo yaliyompa ushindi
Buyogela.
Licha
ya mambo mengine, Nsanzugwanko alilalamikia mwenendo mbaya na ukiukaji wa
Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, huku akimtuhumu Buyogela kuendesha kampeni chafu,
kwa kutoa maneno ya kashfa dhidi yake, kuwa ni mchawi aliyeua watu na mwizi.
Alidai kwenye mikutano yake, Buyogela alimtuhumu kuwa aliwaua Wabunge wa zamani
wa jimbo hilo, Bernard Machupa na Teddy Magayane.
Hivyo,
aliomba mahakama hiyo itengue matokeo yaliyompa ushindi na kuamuru ufanyike
uchaguzi mdogo, au imtangaze yeye kuwa mshindi. Hata hivyo, Mei 3, 2012,
Mahakama Kuu Kanda ya Tabora katika hukumu yake iliyotolewa na Jaji Haruna
Songoro, alitupilia mbali madai ya Nsanzugwanko akisema ameshindwa
kuyathibitisha pasipo mashaka yoyote.
Jopo la Majaji
watatu wa Mahakama ya Rufani; Nathalia Kimaro, Salum Massati na William Mandia,
walikubaliana na hoja za mawakili wa utetezi na kuamua kutupilia mbali rufaa
hiyo.
Habari hii imeandikwa na James Magai wa gazeti la Mwananchi.
No comments:
Post a Comment