Monday, 29 July 2013

NDG. EDO MWAMALALA ATEULIWA KUWA KAMISHINA WA CHAMA MKOANI MBEYA

 
Ndugu Edo Makata Mwamalala (pichani) , ameteuliwa kuwa Kamishna wa chama cha NCCR Mageuzi mkoa wa Mbeya.

Barua ya uteuzi wa Mwamalala ya Julai 15, mwaka huu yenye kumbukumbu namba NCCR-M/MM/UTV/102, inesema kuwa Mwenyekiti wa chama Taifa amemteua kuwa Kamishna wa chama katika mkoa huo.

"Napenda kukutaarifu kuwa, kwa mamlaka na madaraka aliyopewa kwa mujibu wa ibara ya 26(2)(f) na ibara ya 37(7) ya Katiba ya NCCR-Mageuzi, toleo la sita sita kama lilivyohaririwa mwaka 2003, Mwenyekiti wa chama Taifa amekuteua kuwa Kamishna wa chama cha NCCR-Mageuzi mkoa wa Mbeya’’ inasomeka sehemu ya barua hiyo.

Barua hiyo iliyosainiwa na kaimu katibu mkuu Ndg. Mosena J. Nyambabe, na kupelekwa nakala kwa Mkuu wa mkoa wa Mbeya, Kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya na Wenyeviti wa chama, Majimbo yote ya mkoa wa Mbeya.

Edo Mwamalala, amekiri kupata barua hiyo Julai 25, mwaka huu.

‘’Ni kweli nimepata barua ya uteuzi na ninatarajia kukutana na waandishi wa habari kueleza nia ya chama changu kufanya ziara katika mkoa wa Mbeya’’ alisema Mwamalala.
 
Habari hii imeandikwa na Dordon Kalulunga.
 
Tunampongeza na kumtakia kila la heri katika majukumu yake.

No comments:

Post a Comment