Thursday, 10 January 2013

SHUKRANI KWA KUTEULIWA


 
(Deogratius Kisandu wakati ikipokea Kadi ya NCCR-Mageuzi. Kulia kwake ni Kaimu Katibu Mkuu Ndugu Faustin Sungura)

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
YAH: SHUKRANI KWA KUTEULIWA

Kwanza natoa shukurani zangu  za dhati, kwa Katibu Mkuu wa Kitengo cha Vijana wa NCCR-Mageuzi  Ndugu Ojung Seitabau, kuniteua kuwa  Katibu wa Mahusiano na Uenezi Taifa, kitengo cha vijana.
Baada ya uteuzi huu wa heshima kwangu, ninaahidi kwamba nitafanya kazi kwa kushirikiana na wenzangu ili kutimiza azma yetu na kutekeleza malengo yafuatayo:-

1. Kuendeleza  kauli mbiu ya vijana ya  "VIJANA NI RASILIMALI YA TAIFA";
lengo kuu ni kuwasha indiketa kwa vijana kwamba milango sasa iko wazi katika kulitumikia Taifa, na kazi ya ukombozi wa pili wa Taifa hili iko mikononi mwetu, na tusikubali kufanya maandamano ambayo hatujui malengo yake na au hatukuyaandaa pamoja.

2. Kuandaa  baadhi ya wagombea vijana wa Ubunge na Udiwani kwa  mwaka 2015 kupitia idara ya vijana nchi nzima.

3. Kufanya  uhamasishaji wa chama katika majimbo yote  kwa nchi nzima.
4. Kuimarisha  TASK FORCE YA USHINDI kwa vijana hususan katika majimbo tutakayogombea .

Ahsanteni sana,

Deogratius Kisandu
KATIBU WA MAHUSIANO NA UENEZI TAIFA, KITENGO CHA VIJANA WA NCCR-Mageuzi
10/01/2013

No comments:

Post a Comment