Monday 7 January 2013

NCCR- MAGEUZI WAWASILISHA MAONI YA KATIBA MPYA

Na Florian Rutayuga Mbeo
Chama cha NCCR-Mageuzi kikiongozwa na Mwenyekiti wake wa Taifa Ndugu James Francis Mbatia (Mb), kimewasilisha maoni yake juu  ya Katiba Mpya tarajiwa, leo tarehe 7-1-2013, kuanzia saa 7:00 mch. hadi saa 8:14 mch.; mbele ya jopo la wajumbe wa Tume, wakiongozwa Mwenyekiti wa Tume hiyo Jaji mstaafu, Ndugu Joseph Sinde Warioba na Naibu Katibu wa Tume hiyo.
Katika kuwasilisha, hoja za NCCR, Ndugu Mbatia  na ujumbe wake wameeleza masuala ya msingi ambayo hayana budi kuzingatiwa/kuwemo katika katiba mpya ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.
Masuala hayo ni  pamoja na:
  • Ukuu wa Katiba
  • Uraia na utaifa
  • Lugha ya Taifa
  • Mji mkuu
  • Muundo wa serikali
  • Muafaka wa kitaifa
  • Uhuru na haki za binadamu
  • Uhuru wa vyombo vya habari
  • Uhusiano wa kimataifa
  • Wajibu wa mwananchi  kwa taifa lake
  • Haki ya kuchagua na kuchaguliwa
  • Haki ya vyama vya siasa
  • Sera elekezi, katika maadili na misingi ya taifa
  • Tume huru ya uchaguzi
  • Kushitakiwa na kutoshitakiwa kwa Rais
  • Muda wa kushika nafasi ya urais
  • Masharti ya ofisi ya Rais
  • Mshahara na marupurupu ya Rais
  • Kumuondoa Rais madarakani (Sababu za kumuondoa rais madarakani, Namna ya kumuondoa Rais madarakani)
  • Kura ya kutokuwa na imani na kiongozi
  • Wananchi kumwondoa mbunge/diwani katika uongozi
  • Maadili na miiko ya uongozi
  • Mamlaka ya Rais ya kuteua
  • Muundo wa utwala
  • Baraza la mawaziri
  • Rasilimali za taifa
  • Madai dhidi ya serikali
  • Mahakama maalum ya katiba
  • Baraza la vijana 
  • Baraza la wazee 
  • Madaraka ya umma ( Decentralization of power)
  • Ardhi
  • Marekebisho ya katiba
  • Mapendekezo kuhusu mambo ya shirikisho.
  • n.k.
Hizo ndizo ajenda muhimu zilizowasilishwa na Chama cha NCCR-Mageuzi. Aidha, Mbatia pamoja na wanamageuzi alioambatana nao walifafanua hoja hizo kwa urefu na mapana na kueleza misingi (justification) ya kwa nini Chama cha NCCR kimeanisha hoja hizo hapo juu.

Itakumbukwa kwamba chama hiki chimbuko lake (mwaka 1991) ni madai ya katiba mpya. Hoja zilizowasilishwa zilikuwa katika fikira za wanamageuzi tangia enzi hizo. Hivyo tarehe hii inaingia katika kumbukumbu za chama kama fursa nyingine ya kuhakikisha lengo hili la msingi la chama, lenye maslahi kwa nchi hatimaye linafikiwa.

No comments:

Post a Comment