Mwenyekiti wa Tume ya mabadiliko ya Katiba Jaji Joseph Warioba akiongea katika mkutano na uongozi wa NCCR-Mageuzi uliofika ofisi za Tume kuwasilisha maoni ya chama hicho kuhusu Katiba Mpya leo (Jumatatu, Jan 7, 2013) jijini Dar es Salaam. Katikati ni Katibu wa Tume Ndg. Assaa Rashid na kushoto ni Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi James Mbatia.
Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi Ndg. James Mbatia akiongea katika mkutano na Tume ya Mabadiliko ya Katiba wakati chama chake kilipokwenda katika ofisi za Tume jijini Dar es Salaam leo (Jumatatu, Jan 7, 2013) kuwasilisha maoni ya chama hicho kuhusu Katiba Mpya. Kulia ni Mwenyekiti wa Tume hiyo Jaji Joseph Warioba na katikati ni Katibu wa Tume Ndg. Assaa Rashid.
Baadhi ya viongozi wa NCCR-Mageuzi wakifuatilia mkutano kati ya chama chao na Tume ya Mabadiliko ya Katiba leo (Jumatatu, Jan. 7, 2013) wakati chama hicho kilipowasilisha maoni kuhusu Katiba Mpya.