Tuesday, 2 October 2012

UONGOZI WA CHAMA WAELEKEA ARUSHA MSIBANI

Uongozi wa chama chini ya Mwenyekiti wa Taifa Ndugu James Francis Mbatia, umeondoka leo jijini Dar es Salaam kuelekea mkoani Arusha kwa ajili ya mazishi ya aliyekuwa mmoja wa waasisi wa chama chetu (NCCR-Mageuzi). Maziko yatafanyika kijijini kwake Oljilaj wilayani Arumeru.
Uongozi huo, umeondoka katika uwanja wa ndege wa mwalimu Julius Kambarage Nyerere, mnamo saa tano asubuhi. Ndg. Mbatia ameambana na Ndg. Nderakindo Kessy (Mbunge wa Afrika Mashariki). Vingozi wengine watakaoungana na ujumbe huu ni pamoja na Ndg. Rakia Abubakar (Makamu Mwenyekiti), Ndg. Mariam Mwakingwe (Mweka hazina- taifa),  Ndg. Laurent Surumbu Tara (Naibu Katibu Mkuu), na Ndg. Victor Sule (Kamishna wa chama mkoa wa Manyara).
Marehemu Ole-Sirikwa (pichani) aliaga dunia tarehe 28-09-2012.


Chama kinawaomba wananchi wa mkoa wa Arusha bila kujali itikadi zao wajitokeze kwa wingi kumuaga mzee wetu Emmanuel Petro Ole-Sirikwa anapoelekea katika pumziko lake la milele.

No comments:

Post a Comment