Thursday, 24 May 2012

ZIARA YA CHAMA MIKOA YA MTWARA NA LINDI

Uongozi wa Kitaifa wa Chama uko katika ziara ya siku kumi kusini mwa nchi, katika mikoa ya Mtwara na Lindi, hususan wilaya za Tandahimba, Nanyumbu na Liware.
Katika ziara hiyo, yupo Mwenyekiti-Taifa, Ndg. James Mbatia (MB), Ndg. Felix Mkosamali (MB), Ndg. Martin Juju Danda (Msaidizi wa Mwenyekiti) na Ndg. Hamad Msabaha (Mjumbe wa Halmashauri Kuu).
Mpaka sasa kutokana na ziara hiyo, jumla ya wanamageuzi wapya 1900 wamejiunga na chama, na matawi mapya zaidi ya 10 yamefunguliwa.
Ziara inatarajiwa kumalizika mnamo tarehe 31 Mei, 2012.
Shime PAMOJA TUTASHINDA!

No comments:

Post a Comment