Friday, 30 August 2013

MAONI YA NCCR-MAGEUZI KUHUSU KATIBA MPYA

NCCR-MAGEUZI WAWASILISHA MAONI YA KATIBA MPYA

Chama cha NCCR-Mageuzi leo tarehe 30/08/2013 kimewasilisha maoni kiliyoyakusanya kupitia kwa wanachama na mashabiki wake  kwa kutumia mikutano mbalimbali chini ya kifungu cha sheria Na. 18(1) na (6) Sura ya 83 ya Mabadiliko ya Katiba.
Kwa mujibu wa vifungu hivyo hapo juu, NCCR-Mageuzi ilikuwa baraza la kukusanya maoni kutoka kwa wanachama wake.
Kabla ya kuwasilisha maoni hayo, Kaimu Katibu Mkuu wa Chama hicho Ndugu Mosena J. Nyambabe, alizungumza naWanahabari, ambapo aliwaeleza wanahabari hao kuwa, Chama  kimefurahishwa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba kwa kuingiza mapendekezo ya NCCR-Mageuzi katika Rasimu hiyo kwa zaidi ya 80%.
Alionesha ibara mbalimbali zilizowekwa na Tume hiyo katika Rasimu hiyo ambazo zinaendana na mapendekezo ya NCCR-Mageuzi.


No comments:

Post a Comment