Friday, 1 March 2013

HATUA ZA DHARURA ZA KUOKOA ELIMU YA TANZANIA


Ndugu James F. Mbatia (Mb) akimkabidhi Mhe. Rais Jakaya M. Kikwete  mojawapo ya mapendekezo yaliyopata kutolewa na Chama cha NCCR-Mageuzi .
Leo tarehe 1 Machi, 2013 Chama cha NCCR-Mageuzi kimepeleka mapendekezo yake kwa Mheshimwa Dk. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kikimwomba pamoja na mambo mengine achukue hatua za dharura kuinusuru elimu ya Tanzania. Hatua hiyo inakuja baada ya hoja ya Mbunge na Mwenyekiti wa Chama hiki - Taifa, Ndugu James Mbatia kupeleka hoja bungeni juu ya udhaifu wa elimu nchini, iliyofuatiwa na matokeo mabaya ya mtihani wa kidato cha nne, siku chache baadaye.
Habari hii ni kwa mujibu wa maafisa wa chama walioko makao makuu ya chama, jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment