Thursday 24 January 2013

WAZEE WA MIKINDANI MTWARA WAFIKA DAR ES SALAAM KUZUNGUMZIA SUALA LA GESI

Pichani: Wazee kumi kutoka Mkoani Mtwara wakiwa wanaingia kwenye ukimbi wa Mikutano wa Maelezo jijini Dar es Salaam leo wakiwawakilisha wanamtwara kwa ajili ya kuja kutoa Tamko lao kuhusiana na Gesi iliyogundulika Mkoani kwao.

Wazee wa  Mtwara Mikindani leo wameongea na waandishi wa habari katika ukumbi wa habari Maelezo kuelezea matakwa yao kwa Serikali juu ya suala zima la Gesi ambayo inapatikana katika Mkoa wao.
Akizungumza kwa niaba ya wazee wenzake,  Mzee Selemani Mademu amesema kuwa wanaitaka Serikali kuhakikisha kuwa Gesi inawafaidisha wao kwanza kabla ya kwenda kuwafaidisha wengine.
Amesema kuwa  wao wametumia Gharama zao wenyewe ikiwa ni pamoja na kuuza Mbuzi wao ili wapate nauli ya kuja kuitetea Gesi yao kwa manufaa ya wanamtwara wote kwa Ujumla.
Ameendelea kusema kuwa, wanaitaka serikali ihakikishe kuwa kituo cha kusafishia Gesi kinajengwa mkoani Mtwara kwani kuna bandari yenye kina kirefu kwa ajili ya Kazi hiyo na amesema kuwa wanaitaka serikali  katika kutekeleza    swala hilo ifanye vitendo kwanza na sio ahadi kama ilivyozoeleka.
“Tumechoshwa na ahadi za Serikali na kwa hili hatuhitaji tena ahadi tunataka vitendo la sivyo Gesi haitoki Mtwara tutazidi kuandamana, tuna rekodi ya ahadi tulizoahidiwa na Serikali na hazijatekelezwa mpaka leo kama vile: Barabara, Umeme, kuimarishwa kwa Bandari,  Mikopo  kwa ajaili ya Ujasiriamali, viwanda vidogo kwa ajili ya Kubangua korosho  n.k. kwa hivyo sisi tunataka vitendo tu, tushachoshwa na ahadi”, Amesema Mademu.
Serikali pia imetakiwa, kutimiza ahadi ya kujenga viwanda kama vya Mbolea na Saruji kama ilivyo ahidi kwa wanaMtwara jambo ambalo litawapa Matumaini  yasiyokuwa na Shaka kuhusu kupata Ajira, pamoja na kuratibu mchakato mzima wa Matumizi ya Gesi kwa kuwashirikisha mikoa ya kusini kwa hatua Zote na kwa uwazi.Aidha wameitaka Serikali kujenga kituo cha kufua Umeme Power Plant Mtwara.
Wazee hao pia wamekanusha taarifa zinazomhusu Mwenyekiti wa NCCR-MAGEUZI  Mhe, James Mbatia za kuwa alishushwa jukwaani tarehe 13/01/2013 na kusema kuwa jambo hilo halina ukweli wowote.

No comments:

Post a Comment