Saturday, 1 December 2012

MAENDELEO YA ZIARA YA VIONGOZI MIKOANI

 NCCR-MAGEUZI WAENDELEA KUFANYA ZIARA MIKOANI

Viongozi wa kitaifa wa NCCR-Mageuzi, wanaendelea vizuri na ziara katika mikoa mbalimbali nchini. Kwa sasa wako katika Mkoa wa Manyara, Jimbo la Babati Vijijini.
Walio katika msafara huo wa viongozi, ni Ndugu Peterson W. Mushenyera (Kamishna wa chama wa Mkoa wa Kagera), Ndugu Juju Martin Danda (Mjumbe wa NEC ya chama na msaidizi wa Mwenyekiti), Ndugu Hemed Msabaha (Mjumbe wa NEC ya chama), Ndugu Beati Mpitabakana (Mjumbe wa NEC na Mhasibu wa chama), Ndugu Victor J. Sulle (Kamishna wa chama wa Mkoa wa Manyara ). Viongozi hawa kwa sasa wanaambatana na Viongozi wa Jimbo la  Babati Vijijini.
Habari zilizotufikia katika blog hii, ni kwamba ziara za mikoani zimekuwa za mafanikio makubwa sana kichama. Hakika NCCR-Mageuzi inazidi kuwa imara. Wananchi wengi wanazidi kujiunga katika chama baada ya kusikia wenyewe sera nzuri za chama zinazotajwa majukwaani na viongozi wetu hawa. Wengi wamesikika wakisifia ubora wa sera hizo hasa wakiangalia jinsi zilivyosheheni hoja za utu, amani, mageuzi na maendeleo.
Shime pamoja tutashinda.  

No comments:

Post a Comment