Tuesday, 29 May 2012

ZIARA YA CHAMA MKOANI LINDI

Baada ya kumaliza ziara mkoani Mtwara kwa mafanikio ya kupata wanachama wengi wapya, kutangaza sera za chama na kufungua matawi mapya, sasa kazi hiyo imeamia mkoani Lindi. Tunavishukuru vyombo vya habari vinavyoendelea kuripoti ziara yetu. Mojawapo ya vyombo hivyo ni gazeti la Majira ambalo leo linaripoti kama ifuatavyo:
NCCR JINO KWA JINO NA CCM
Na Mwandishi Wetu, Lindi

MSHAURI Mkuu wa Mwenyekiti wa Chama cha NCCR-Mageuzi Bw. James Mbatia, Danda Juju ambaye pia ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya chama hicho amesema ni hatari wananchi kubadili mitazamo yao kisiasa kutokana na maisha magumu yanayowakabili.


Alisema, kama Chama Cha Mapinduzi (CCM) hakitaki kuondoka madarakani kwa hiari, siku wananchi wakiamua kukiondoa madarakani machafuko yanaweza kutokea.

Hayo aliyasema jana Mjini Liwale Mkoa wa Lindi,alipokuwa akihutubia mkutano wa hadhara.

"Hiki Chama Cha Mapinduzi kimechoka, nasema kimechoka kweli kweli na hakina tena sifa za kutawala nchi hii ingawa viongozi wake hawataki kulikubali hilo.

"Sisi hatutaki kufika huko, Tanzania ni nchi ya amani, Tanzania ndiyo nchi inayoheshimika duniani kwa amani na utulivu, lakini narudia tena, binadamu anapobadilika kwa sababu ya shida zinazomkabili anakuwa mbaya zaidi kuliko hata mnyama," alisema Mjumbe huyo wa Halmashauri Kuu ya NCCR-Mageuzi.

Wakati huo huo, alisema CCM ya sasa siyo CCM ya kuwavutia watu kwa sababu chama hicho hakifuati misingi ya utawala bora na kwamba ili kuondokana na kero zinazosababishwa na utawala wa chama hicho wananchi hawana budi kukikataa kwa vitendo

No comments:

Post a Comment