Monday, 28 May 2012

Matawi Mengine Mapya ya Chama Yafunguliwa Mkoani Mtwara

Kwa Mujibu wa gazeti la Majira la t. 28/05/2012
MWENYEKITI wa Chama cha NCCR-Mageuzi Bw. James Mbatia amesema bei ya zao la korosho imepanda kutokana na jitihada za chama chake na kuahidi kuendelea kuwapigania wakulima.
Bw. Mbatia alitoa kauli hiyo kwa nyakati tofauti juzi mkoani Mtwara alipokuwa akifungua matawi ya chama hicho katika Jimbo la Mtwara Mjini.
Aliongeza kuwa, baadhi ya watu wanaweza wasikubaline na hilo, lakini ukweli ni kwamba wakulima wa zao hilo katika mikoa ya Mtwara na Lindi wanalipwa sh. 1,200 kwa kilo kutokana na jinsi chama hicho kilivyokuwa kikiwatetea kwa nguvu wakulima hao.
Alisema, wananchi wa Mtwara wamesahaulika wakati wanalima korosho na ufuta kwa kuwa fedha wanazolipwa ni kidogo.
Aliongeza kuwa Machi, mwaka huu, alikuwa mkoani humo, ambapo  alishangaa kusikia wapata hasara. "Niliposikia hivyo, nikachachamaa, hadi bei ya zao la korosho ikapanda," alisema.
“Pamoja na kuandika barua kwa rais, tuliendelea kupiga kelele kila siku na hatimaye kelele zetu zimekuwa mkombozi kwa wana Mtwara na Lindi kwa sababu sasa naambiwa mnalipwa sh. 1,200 kwa kilo moja ya korosho," alisema.
Alisisitiza kuwa fedha hizo bado hazitoshi, wanataka walipwe zaidi ya kiasi hicho kwa sababu maisha ni magumu.
Katika ziara yake hiyo, Bw. Mbatia alifungua tawi katika Kijiji cha Namayanga pamoja na matawi mawili katika Kata ya Likombe likiwamo Tawi la Likombe na Tumaini Jema.
Pia alifungua Ofisi ya Kata ya Majengo, alifungua Tawi la Mbatia, lililoko Kata ya Ufukoni, alifungua Tawi la Uledi lililoko Kata ya Chikongola na pia mwanasiasa huyo alifungua Tawi la Harakati lililoko Chikongora

No comments:

Post a Comment