Wednesday, 30 May 2012

Tumepata Wanachama Wapya 2517 Mtwara Mjini

Katika ziara inayoendelea mkoani Mtwara, hadi sasa wanachama wapya 2,517 wamejiunga na chama katika Jimbo la Mtwara Mjini.
Takwimu hizi ni kwa mujibu wa Mjumbe wa Halmashauri ya chama Ndg. Danda Juju, ambaye alizitoa alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari mjini Mtwara.
Alisema kuwa, idadi hiyo imepatikana kutokana na jitihada za uhamasishaji ambazo zimekuwa zikifanywa na viongozi wa kitaifa na wa jimbo hilo.
“Chama kinazidi kushika kasi, tumekuwa tukipata wanachama wapya kila kunapokucha kwa sababu wananchi wametambua kuwa NCCR-Mageuzi ndicho chama makini kitakachoweza kuwakomboa.
Tumepata wanachama wengi na tunaamini idadi itazidi kuongezeka kwa sababu wananchi wa Mtwara wameshaamka, na wanataka mageuzi hasa kutokana na kukichoka chama tawala,”
Kwa mujibu wa Juju ambaye pia ni Msaidizi Mkuu wa Mwenyekiti wa chama hicho Bw. James Mbatia;  baadhi ya wanachama wanaojiunga na chama wanatoka vyama vingine vya siasa.

No comments:

Post a Comment